Processing...

News Room

MARADI WA THEATER WAPEWA BARAKA NA MWENGE

MARADI WA THEATER WAPEWA BARAKA NA MWENGE
MARADI WA THEATER WAPEWA BARAKA NA MWENGE
MARADI WA THEATER WAPEWA BARAKA NA MWENGE
+3 More Images
MARADI WA THEATER WAPEWA BARAKA NA MWENGE
MARADI WA THEATER WAPEWA BARAKA NA MWENGE
Wataalamu wa afya na lishe kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC pamoja na Chuo Kikuu KCMC nao wameungana katika maadhimisho ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa lishe bora katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza. Kupitia tafiti mbalimbali zilizofanywa na KCMC kwa kushirikiana na Chuo Kikuu KCMC, imebainika kuwa ulaji wa vyakula vya asili vyenye virutubisho sahihi na vilivyoandaliwa kwa njia bora una mchango mkubwa katika kuboresha afya na kupunguza hatari ya magonjwa yasiyoambukiza. Wananchi wamehimizwa kuendelea kuthamini na kutumia vyakula vya asili kama sehemu ya maisha yao ya kila siku kwa ajili ya kujenga jamii yenye afya bora. Sambamba na utoaji wa elimu hiyo, wataalamu wa lishe wameeleza mafanikio ya KCMC katika utoaji wa huduma za lishe tiba, ikiwemo utayarishaji wa Total Parenteral Nutrition (TPN), lishe maalumu inayotolewa kwa njia ya mshipa kwa wagonjwa wasioweza kutumia mfumo wa kawaida wa mmeng'enyo wa chakula. Huduma hii imeendelea kuwapa matumaini wagonjwa wenye mahitaji maalumu ya lishe, wakiwemo watoto wachanga, wagonjwa wa upasuaji mkubwa, wagonjwa wa saratani na wengine wenye changamoto mbalimbali za kiafya. KCMC inaendelea kutumia tafiti, ubunifu na elimu ya afya kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya kwa wakati.

Related Stories

MARADI WA THEATER WAPEWA BARAKA NA MWENGE
2026-07-02 00:00:00

MARADI WA THEATER WAPEWA BARAKA NA MWENGE

READ ARTICLE
KCMC YAAMTUNUKU TUZO YA HESHIMAA
2026-06-24 00:00:00

KCMC YAAMTUNUKU TUZO YA HESHIMAA

READ ARTICLE
MHE. RAISI AKIPATIWA MAELEZO KUHUSU VIFAA VYA TIBA MIONZI
2026-06-24 00:00:00

MHE. RAISI AKIPATIWA MAELEZO KUHUSU VIFAA VYA TIBA MIONZI

READ ARTICLE

Join the Discussion

× Preview
🫀
CHANGIA JENGO LA MOYO
Saidia Ujenzi wa Cardiovascular Centre