MAHAFALI YA 105 YA CPE YAFANYIKA KCMC
Leo, tarehe 20 Novemba 2026, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC imeadhimisha mahafali ya 105 ya Kituo cha Ushauri na Utunzaji wa Kichungaji (Clinical Pastoral Education – CPE), ambapo jumla ya watumishi 31 wamehitimu mafunzo hayo.
Mahafali hayo yameongozwa na Mchungaji Laretoni Loishiye Lukumay, Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea watumishi ujuzi na uwezo wa kutoa huduma ya ushauri nasaha, faraja ya kiroho na utunzaji wa kichungaji kwa wagonjwa, ndugu wa wagonjwa pamoja na jamii kwa ujumla.
Kupitia mafunzo hayo, wahitimu wamejengewa uwezo wa kuelewa mahitaji ya wagonjwa kwa mtazamo mpana unaozingatia afya ya mwili, akili na roho, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha huduma jumuishi na zenye utu kwa wagonjwa.
KCMC inaendelea kuwekeza katika kuwaimarisha watumishi wake kupitia mafunzo mbalimbali yanayolenga kuboresha ubora wa huduma na kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma zinazozingatia mahitaji yao ya kimwili, kihisia na kiroho.
Related Stories