KCMC & HEALTHSERV GLOBAL KUIMARISHA HUDUMA ZA WAZEE
Katika kuendeleza na kuboresha huduma za afya kwa wazee (Geriatrics Services), Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC imepokea ugeni wa Bi. Jenny Chapman, Mjumbe wa Bodi ya Shirika la HealthServ Global, shirika lisilo la kiserikali kutoka nchini Australia, kwa ajili ya mazungumzo kuhusu maendeleo ya huduma za afya kwa wazee.
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili fursa za ushirikiano katika kuimarisha huduma za kibingwa zinazozingatia mahitaji ya wazee, pamoja na kuboresha ustawi na ubora wa maisha yao.
Pichani, Bi. Jenny Chapman akiwa pamoja na Prof. Michael Burke, Mtaalamu wa Magonjwa ya Wazee na Tiba ya Familia (Geriatrics & Family Medicine), akiongozana na viongozi wawili wa KCMC walioshiriki katika mazungumzo hayo, ambao ni Dkt. Sarah Urasa, Mkurugenzi wa Tiba, na Bi. Brenda Kitali, Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi.
Related Stories