PROF. MASENGA AFUNGUA MAFUNZO YA MAGONJWA YA MFUMO WA CHAKULA
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini - KCMC leo, tarehe 26 Oktoba 2026, imefungua rasmi kambi ya mafunzo maalumu na warsha kuhusu magonjwa ya mfumo wa chakula, Endoskopi na Patholojia, katika Ukumbi wa Maktaba wa KCMC. Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Prof. Gileard Masenga.
Mafunzo hayo ya siku tano, yanayotarajiwa kuhitimishwa tarehe 30 Oktoba 2026, yameandaliwa kwa kushirikiana na Leiden University Medical Center kutoka Uholanzi, yakilenga kuongeza maarifa na ujuzi wa wataalamu wa afya katika utambuzi na matibabu ya magonjwa ya mfumo wa chakula na ini.
Kupitia mafunzo hayo, washiriki wanapata fursa ya kujifunza mbinu za kisasa za uchunguzi wa Endoskopi na Patholojia, kupitia slaidi za uchunguzi, kushiriki mafunzo ya vitendo na kujadiliana kuhusu changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utambuzi na matibabu ya wagonjwa wenye magonjwa ya mfumo wa chakula.
Warsha hiyo inawakutanisha wataalamu wa afya kutoka ndani na nje ya Tanzania, wakiwemo wawezeshaji kutoka Leiden University Medical Center nchini Uholanzi, huku ushiriki wa wataalamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando ukitarajiwa kuimarisha zaidi ubadilishanaji wa uzoefu na maarifa ya kitaalamu.
Related Stories