KCMC YAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA YA AFYA
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini - KCMC imepokea ugeni kutoka World Vision Tanzania ukiambatana na wawakilishi wa Serikali ya Marekani kwa lengo la kufanya mazungumzo ya kitaalamu na kujifunza uzoefu wa KCMC katika utoaji wa huduma za afya.
Ziara hiyo ni sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wa Mpango wa Imani na Jamii (Faith & Community Initiative – FCI), unaolenga kuimarisha mifumo ya afya inayotegemea taasisi za kidini na jamii, pamoja na kuongeza ushirikiano kati ya wahudumu wa afya na jamii ili kuboresha upatikanaji wa huduma jumuishi za afya.
Katika ziara hiyo, wageni wamepata fursa ya kujifunza uzoefu wa KCMC katika utoaji wa huduma za rufaa, ushauri wa kitaalamu na mafunzo ya hospitali. Aidha, walijadili mifumo ya utoaji huduma za afya, ushirikiano na wadau, mifumo ya rufaa, pamoja na fursa za kuimarisha huduma za afya zinazowafikia wananchi kwa ufanisi.
Related Stories