KCMC NA TVOH YAWAANGAZIA WENYE JINSI TAT
Leo, tarehe 8 Septemba 2026, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini KCMC imepokea ugeni kutoka Tanzania Voice of Humanity (TVOH) @tanzaniavoiceofhumanity katika ziara yenye lengo la kuimarisha ushirikiano katika kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii.
Katika ziara hiyo, KCMC na TVOH zimekabidhiana Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) kwa ajili ya kuanzisha huduma ya ushauri nasaha kwa watoto na watu waliozaliwa na jinsi tata (Intersex/DSD). Huduma hiyo inalenga kutoa msaada wa kitaalamu, kisaikolojia na kijamii kwa watoto, watu wenye hali ya Intersex/DSD pamoja na familia zao, ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali na kupata huduma kwa heshima, utu na bila unyanyapaa.
Tanzania Voice of Humanity (TVOH) ni taasisi inayojikita katika kutetea haki, kutoa elimu, kuongeza uelewa wa jamii na kusaidia ustawi wa watu wenye Intersex, watu wenye ulemavu na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu. Kupitia programu zake, TVOH huchangia kupunguza unyanyapaa na ubaguzi, kuhamasisha upatikanaji wa huduma muhimu, pamoja na kuwawezesha watu na jamii kutambua na kudai haki zao.
KCMC inaendelea kuthamini na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali kama TVOH katika kuhakikisha kila mtu anapata huduma bora za afya bila ubaguzi.
Related Stories