Processing...

News Room

SNAKE ANTIVENOM ZAFIKA KCMC

SNAKE ANTIVENOM ZAFIKA KCMC
SNAKE ANTIVENOM ZAFIKA KCMC
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini - KCMC imepokea msaada wa dawa ya Snake Antivenom kutoka Meserani Snake Park Clinic, chini ya uongozi wa Dkt. Jonas Nickel na kuwasilishwa na Mkuu wa Idara ya Dharura na Ajali - KCMC Dkt. Francis Sakita (wapili kutoka mkono wa kulia). Dawa hiyo hutumika katika matibabu ya watu waliong’atwa na nyoka wenye sumu, kwa kusaidia kupunguza na kuzuia madhara makubwa yanayosababishwa na sumu hiyo mwilini. Upatikanaji wa dawa hii ni muhimu katika kuokoa maisha na kupunguza hatari ya madhara makubwa kwa wahanga wa kung’atwa na nyoka. Msaada huu unaendelea kuimarisha ushirikiano mzuri kati ya KCMC na Meserani Snake Park Clinic katika kuhakikisha wahanga wa kung’atwa na nyoka wanapata matibabu stahiki na kwa wakati. KCMC inaendelea kuthamini ushirikiano na wadau mbalimbali katika kuimarisha huduma za afya na kuokoa maisha ya jamii.

Related Stories

NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D
2026-09-16 00:00:00

NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D

READ ARTICLE
KCMC NA TVOH YAWAANGAZIA WENYE JINSI TAT
2026-09-08 00:00:00

KCMC NA TVOH YAWAANGAZIA WENYE JINSI TAT

READ ARTICLE
KCMC, EGPAF ZAJADILI AFYA YANGU
2026-09-07 00:00:00

KCMC, EGPAF ZAJADILI AFYA YANGU

READ ARTICLE

Join the Discussion

× Preview
🫀
CHANGIA JENGO LA MOYO
Saidia Ujenzi wa Cardiovascular Centre