Processing...

News Room

TANNA KCMC YAWASHA MSHUMAA WA UPENDO 2026

TANNA KCMC YAWASHA MSHUMAA WA UPENDO 2026
TANNA KCMC YAWASHA MSHUMAA WA UPENDO 2026
TANNA KCMC YAWASHA MSHUMAA WA UPENDO 2026
+3 More Images
TANNA KCMC YAWASHA MSHUMAA WA UPENDO 2026
TANNA KCMC YAWASHA MSHUMAA WA UPENDO 2026
Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC, leo tarehe 29 Mei 2026, wameadhimisha kilele cha Siku ya Kimataifa ya Wauguzi Duniani, ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Mei, kupitia shughuli mbalimbali zilizolenga kuthamini mchango wa wauguzi katika utoaji wa huduma za afya. Maadhimisho hayo yalihusisha utoaji wa pongezi kwa wauguzi wastaafu pamoja na zoezi la kuwasha taa ya upendo, ikiwa ni ishara ya kuenzi na kuendeleza misingi ya huruma, utu, uvumilivu na kujitolea iliyoasisiwa na mwanzilishi wa taaluma ya uuguzi duniani, Bi Florence Nightingale. Wauguzi walihimizwa kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa kwa weledi, maadili na upendo kwa kuzingatia viwango vya taaluma yao. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya KCMC, Prof. Gileard Masenga, alieleza kuwa wauguzi ni nguzo muhimu katika mfumo wa huduma za afya kutokana na nafasi yao kubwa katika kutoa huduma, faraja na matumaini kwa wagonjwa pamoja na familia zao katika kipindi chote cha matibabu na uponyaji.

Related Stories

KCMC NA TVOH YAWAANGAZIA WENYE JINSI TAT
2026-09-08 00:00:00

KCMC NA TVOH YAWAANGAZIA WENYE JINSI TAT

READ ARTICLE
KCMC, EGPAF ZAJADILI AFYA YANGU
2026-09-07 00:00:00

KCMC, EGPAF ZAJADILI AFYA YANGU

READ ARTICLE
BANDA LA KCMC LAVUTIA WAGENI ARUSHA
2026-08-27 00:00:00

BANDA LA KCMC LAVUTIA WAGENI ARUSHA

READ ARTICLE

Join the Discussion

× Preview
🫀
CHANGIA JENGO LA MOYO
Saidia Ujenzi wa Cardiovascular Centre