Processing...

2026-04-01 00:00:00 SARATANI 5 min read

MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI YASHIKA KASI: KCMC YAZINDUA KAMATI MAALUM

Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
*Moshi, Kilimanjaro* Katika hatua muhimu ya kuimarisha mapambano dhidi ya saratani nchini, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC imezindua rasmi Kamati ya Ushauri ya Rejesta ya Saratani Mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha ukusanyaji, uhifadhi na matumizi ya takwimu sahihi za ugonjwa huo. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mratibu wa Huduma za Saratani nchini, Dkt. Caroline Mrema, alieleza kuwa uanzishwaji wa rejesta ya saratani ni hatua muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi zitakazosaidia kupanga mikakati madhubuti ya kudhibiti na kupunguza athari za ugonjwa huo. Alibainisha kuwa kwa muda mrefu kumekuwepo na changamoto ya upatikanaji wa takwimu kamilifu na zenye kuaminika kuhusu saratani, hali inayosababisha ugumu katika kupanga huduma, kugawa rasilimali pamoja na kufanya tafiti zenye tija. Hata hivyo, alisisitiza kuwa kupitia mfumo huu wa rejesta, nchi itaweza kuwa na msingi imara wa data utakaoongoza maamuzi ya kisera na kitaalamu. Dkt. Mrema aliongeza kuwa rejesta ya saratani siyo tu nyenzo ya kukusanya takwimu, bali ni chombo muhimu cha kusaidia kufuatilia mwenendo wa ugonjwa huo, kubaini maeneo yenye uhitaji mkubwa na kupima ufanisi wa huduma zinazotolewa kwa wagonjwa. Aidha, aliwahimiza wadau wote kushirikiana kwa karibu ili kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ufanisi na endelevu. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Prof. Gileard Masenga, alisisitiza dhamira ya KCMC katika kusimamia ubora wa data za saratani katika Mkoa wa Kilimanjaro. Alieleza kuwa ubora wa data ni msingi muhimu katika mapambano dhidi ya saratani, kwani huwezesha upangaji sahihi wa huduma za afya, matumizi bora ya rasilimali pamoja na uundaji wa mikakati madhubuti ya kudhibiti ugonjwa huo. “Bila kuwa na data sahihi na zenye kuaminika, inakuwa vigumu kufanya maamuzi sahihi ya kitaalamu na kupanga hatua stahiki za kudhibiti na kutibu saratani,” alisisitiza Prof. Masenga. Aidha, aliwahimiza wataalamu wa takwimu pamoja na timu ya Cancer Registry kuendelea kuimarisha ukusanyaji na usimamizi wa taarifa ili kuhakikisha data inayokusanywa inakuwa sahihi, kamilifu na yenye kuaminika wakati wote.

Related News

Medical technology
2026-04-01 00:00:00

MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI YASHIKA KASI: KCMC YAZINDUA KAMATI MAALUM

Read Story →
Medical technology
2026-03-24 00:00:00

MAPAMBANO DHIDI YA LISHE DUNI

Read Story →
Medical technology
2026-03-19 00:00:00

KAMPENI YA UCHANGIAJI KITENGO CHA MOYO - KCMC

Read Story →

Leave a Comment