Processing...

2026-03-24 00:00:00 LISHE 5 min read

MAPAMBANO DHIDI YA LISHE DUNI

Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Mafunzo ya siku tatu ya usimamizi wa lishe duni (malnutrition) yameanza leo rasmi hapa KCMC, yakilenga kuwajengea uwezo wataalamu wa afya katika kuboresha huduma za lishe na matokeo ya wagonjwa. Mafunzo haya ya siku tatu yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Dkt. Sarah Urasa, ambaye alisisitiza umuhimu wa lishe bora katika mchakato mzima wa matibabu na uponyaji wa wagonjwa. Akizungumza wakati wa ufunguzi, Dkt. Urasa alieleza kuwa lishe duni bado ni changamoto kubwa ndani ya mfumo wa huduma za afya, licha ya kuwa ni hali inayoweza kuzuilika na kudhibitiwa kwa urahisi iwapo itagunduliwa mapema. Alifafanua kuwa lishe duni huathiri moja kwa moja kasi ya kupona kwa wagonjwa, huongeza muda wa kulazwa hospitalini, huongeza hatari ya maambukizi na hatimaye kuchangia vifo vinavyoweza kuzuilika. Takwimu zinaonesha kuwa nchini Tanzania, takribani mtoto mmoja kati ya watatu walio chini ya miaka mitano anakabiliwa na udumavu, hali inayodhihirisha changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa lishe bora. Aidha, alibainisha kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, hospitali ya KCMC ilihudumia jumla ya wagonjwa 211 waliokuwa na changamoto za lishe duni, wakiwemo watoto wenye utapiamlo mkali na wa wastani pamoja na udumavu. Hali hii inaonesha wazi kuwa bado kuna haja kubwa ya kuimarisha uelewa na uwezo wa wataalamu wa afya katika kushughulikia tatizo hili kwa ufanisi zaidi. Dkt. Urasa pia alieleza changamoto iliyowahi kujitokeza ya upungufu wa vyakula tiba vilivyokuwa tayari vimetengenezwa (pre-packaged therapeutic feeds), hali iliyosababisha hospitali kubuni suluhisho la kutumia vyakula tiba vinavyotengenezwa kwa kutumia rasilimali za ndani. Kupitia mfumo wa Integrated Management of Acute Malnutrition (IMAM), KCMC imefanikiwa kuendeleza mbinu endelevu ya matibabu kwa kutumia vyakula vinavyopatikana ndani ya jamii, jambo ambalo limeongeza uhakika wa upatikanaji wa huduma hizi muhimu. Mafunzo haya yameandaliwa kwa kushirikisha wataalamu mbalimbali wakiwemo madaktari, wauguzi, wataalamu wa lishe na washiriki kutoka mikoa mbalimbali kama Kilimanjaro, Mara, Manyara, Njombe na Geita. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kitaalamu katika tathmini ya lishe, utambuzi sahihi wa lishe duni, pamoja na usimamizi na utayarishaji wa vyakula tiba kwa kutumia rasilimali zilizopo ndani ya mazingira yao. Katika siku ya kwanza ya mafunzo, washiriki wameanza kwa kufanya utangulizi wa jumla kuhusu lishe duni, wakijifunza tofauti kati ya lishe duni ya muda mfupi (acute malnutrition) na ya muda mrefu (chronic malnutrition), pamoja na athari zake kwa afya ya binadamu. Baada ya hapo, wameendelea na mada ya tathmini ya lishe na utambuzi wake, ambapo wamejifunza mbinu mbalimbali za kitaalamu za kupima hali ya lishe kwa wagonjwa, ikiwa ni pamoja na vipimo vya mwili (anthropometric measurements). Sehemu ya kipekee ya mafunzo ya siku ya kwanza imekuwa ni mazoezi kwa vitendo (role play), ambapo washiriki wamepata fursa ya kufanya tathmini ya vipimo vya mwili kwa vitendo katika vikundi. Zoezi hili limewasaidia washiriki kuunganisha nadharia na vitendo, na hivyo kuongeza uelewa na ufanisi katika utoaji wa huduma halisi kwa wagonjwa. Kwa ujumla, mafunzo haya yanatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko katika utoaji wa huduma za lishe ndani ya hospitali na vituo vya afya, kwa kuweka mkazo katika matumizi ya suluhisho za ndani zilizo endelevu. Uongozi wa KCMC umeweka wazi kuwa mafunzo haya ni mwanzo tu wa safari ya muda mrefu ya kujenga mfumo imara wa huduma za lishe, huku mipango ikiendelea ya kuanzisha mafunzo zaidi, ikiwemo yale yatakayolenga lishe kwa watu wazima.

Related News

Medical technology
2026-03-24 00:00:00

MAPAMBANO DHIDI YA LISHE DUNI

Read Story →
Medical technology
2026-03-19 00:00:00

KAMPENI YA UCHANGIAJI KITENGO CHA MOYO - KCMC

Read Story →
Medical technology
2026-03-13 00:00:00

BAJETI YA 2026/2027 YAWAKUTANISHA

Read Story →

Leave a Comment