WAJUMBE WA BARAZA LA GSF WAJIONEA MIUNDOMBINU YA HOSPITALI
Wajumbe wa Baraza la Shirika la Msamaria Mwema (GSF)/KCMC leo wamefanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya KCMC kwa lengo la kujionea hali ya miundombinu ya hospitali pamoja na namna shughuli na huduma mbalimbali zinavyotekelezwa.
Katika ziara hiyo, wajumbe walipata fursa ya kutembelea maeneo tofauti ya hospitali na kujionea mazingira ya utoaji wa huduma, hali ya majengo na miundombinu inayotumika katika kuwahudumia wagonjwa.
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Baraza la GSF/KCMC katika kufuatilia hali ya taasisi, kutathmini miundombinu iliyopo na kujionea maeneo yanayohitaji kuimarishwa ili kuwezesha utoaji wa huduma bora na salama kwa wagonjwa.
Related Stories
2026-11-04 00:00:00