UZINDUZI WA KLINIKI YA MOYO YA WANAWAKE

Feb 1, 2024

...

Uongozi wa hospitali ya KCMC ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Dkt. Sarah Urasa leo tarehe 1/02/2024 imezindua kliniki mpya ya moyo ya wanawake. Kliniki hii yenye lengo la kufanya uchunguzi na kutibu magonjwa ya moyo kwa wanawake hasa wale wenye ujauzito.

... Hatua hii inaongeza azma ya hospitali ya kutoa huduma za afya zenye ubora na umakini huku tukiendelea kufanya maendeleo katika eneo la tiba na utafiti wa afya ya moyo kwa wanawake