Processing...

Jengo la Matibabu ya Moyo - KCMC

Taasisi ya Shirika la Msamaria Mwema · Moshi

🫀 Taarifa kwa Umma · 09 Aprili 2026

Uchangiaji wa Ujenzi wa Jengo
la Matibabu ya Moyo

KILIMANJARO CHRISTIAN MEDICAL CENTRE – KCMC

TSh 50B

Gharama Zote za Mradi

90%

Ufadhili wa Kimataifa

24,585

Wagonjwa wa Moyo (2020–2025)

102

Vitanda vya Wagonjwa

Kuhusu KCMC

Kilimanjaro Christian Medical Centre – KCMC

Kilimanjaro Christian Medical Centre – KCMC ni hospitali ya Rufaa ya Kanda inayotoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi (consultant and referral specialized hospital) iliyoanzishwa tarehe 06 Machi, 1971 ikihudumia wananchi wa Kanda ya Kaskazini ya Tanzania, inayojumuisha mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Hospitali hii ipo Mkoa wa Kilimanjaro lakini inahudumu wahitaji hata kutoka nje ya mipaka ya eneo lake la rufaa. Kwa zaidi ya miaka 50, KCMC imekuwa nguzo kuu ya afya kwa wananchi wa Tanzania kaskazini na zaidi.

KCMC Logo

KCMC – Tangu 06 Machi, 1971

Taasisi ya Shirika la Msamaria Mwema · Moshi

KCMC Hospital

KCMC – Moshi, Kilimanjaro, Tanzania

Hali Duniani

Magonjwa ya Moyo Kimataifa

Magonjwa yasiyoambukiza (Non-communicable diseases – NCDs) kwa sasa yanachangia takribani asilimia 70 ya vifo duniani. Miongoni mwa magonjwa haya, magonjwa ya moyo na mishipa (cardiovascular diseases – CVDs) ndiyo chanzo kikuu cha vifo.

Magonjwa kama Kiharusi (stroke) na ugonjwa wa kuziba kwa mishipa ya moyo (ischemic heart disease) yanachangia sehemu kubwa ya vifo hivi. Zaidi ya asilimia 78 ya vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza hutokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.

Tofauti na nchi zilizoendelea, katika nchi hizi magonjwa ya moyo huanza kuathiri watu wakiwa katika umri mdogo, hali inayopunguza nguvu kazi na kuathiri maendeleo ya kiuchumi.

Magonjwa ya Moyo Kimataifa
70% ya Vifo Duniani ni NCDs

70%

Vifo vya NCDs Duniani

78%

Vifo vya NCDs – Nchi Maskini

Hali ya KCMC

Magonjwa ya Moyo Hospitali ya KCMC

Magonjwa ya moyo ni miongoni mwa sababu kuu za wagonjwa kulazwa KCMC. Takwimu za hospitali zinaonyesha kuwa asilimia 14.4 ya wagonjwa wanaolazwa ni wagonjwa wa moyo, ambao hulazwa hospitalini kwa wastani wa siku 9 hadi 10. Asilimia 38.5 ya wagonjwa wanaoruhusiwa hulazwa tena baada ya muda.

Kiwango cha vifo kwa wagonjwa wa moyo ni takribani asilimia 18.3 ya vifo vyote vinavyotokea KCMC. Katika kipindi cha miaka mitano (2020–2025), jumla ya wagonjwa 24,585 kati ya 135,136 waliolazwa walikuwa na magonjwa ya moyo.

Aidha, zaidi ya wagonjwa 133,000 kati ya 1,502,236 wa nje walipatiwa huduma za matibabu ya moyo katika kipindi hicho. Hii ni ishara ya ongezeko kubwa la magonjwa ya moyo nchini Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni.

Takwimu za Magonjwa ya Moyo KCMC

14.4%

Wagonjwa wa Moyo wanaolazwa

18.3%

Vifo vya Wagonjwa wa Moyo

24,585

Wagonjwa wa Moyo (2020–2025)

133,000+

Wagonjwa wa Nje (2020–2025)

Lengo la Mradi

Lengo Kuu la Mradi

Katika kukabiliana na ongezeko la magonjwa ya moyo nchini na kuboresha huduma za kibingwa, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC imeanzisha mpango maalum unaojumuisha wazo la kuboresha huduma za moyo, ujenzi wa miundombinu ya kisasa pamoja na kuimarisha kliniki ya moyo.

🎯 Lengo Kuu

Kuanzisha Kituo cha kisasa cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa (fully functional Cardiovascular Centre) katika hospitali ya KCMC kitakachotoa huduma kamili za uchunguzi, matibabu na ufuatiliaji wa wagonjwa wa moyo kwa Kanda ya Kaskazini ya Tanzania na maeneo mengine ndani na nje ya nchi.

💡 "Kuwa jukumu la Afya sio la Serikali tu. Hiyo ndo maana KCMC inataka kuanza huduma hii."

Cardiovascular Centre KCMC

Mfano wa 3D wa Jengo la Cardiovascular Centre

Malengo Mahususi

Malengo Mahususi ya Kituo

Kituo kipya cha Matibabu ya Moyo kitalenga maeneo mbalimbali ya huduma ili kuhakikisha Watanzania wanapata matibabu kamili ya moyo ndani ya nchi yao, na hivyo kupunguza hitaji la rufaa za nje ya nchi.

  • Kuimarisha kinga, kutoa elimu kwa jamii na uchunguzi wa mapema wa magonjwa ya moyo
  • Kuanzisha huduma za kisasa za uchunguzi na matibabu ya moyo
  • Kutoa matibabu ya dawa, matibabu ya kutumia mirija maalum (catheter-based treatment) na upasuaji wa moyo (cardiac surgery)
  • Kutoa huduma za urekebishaji wa afya ya moyo (cardiac rehabilitation) pamoja na ufuatiliaji wa muda mrefu
  • Kupunguza uhitaji wa rufaa za nje ya nchi na mzigo kwa taasisi pekee iliyopo Tanzania
Malengo ya Matibabu ya Moyo
Huduma za Kibingwa
Ujenzi wa Jengo

Jengo la Ghorofa Tatu la Kisasa

Kitengo hiki kitakapokamilika kitakuwa na jengo la kisasa lenye ghorofa tatu litakalojumuisha vyumba na vifaa vya kisasa vya matibabu ya moyo.

🏥 Vyumba 2 vya upasuaji wa moyo (cardiac surgery theatre)
🔬 Maabara 2 za uchunguzi wa mishipa ya moyo (catheterization laboratory)
🛏️ Vyumba vya wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit – ICU) kwa watu wazima na watoto
⬇️ Vitengo vya uangalizi maalum baada ya ICU (step-down ICU units)
🛏️ Vitanda 102 vya wagonjwa wa ndani
🏃 Kliniki za wagonjwa wa nje na kitengo cha urekebishaji wa afya ya moyo (cardiac rehabilitation unit)
🧪 Maabara za uchunguzi na huduma za dawa
Jengo la Matibabu ya Moyo
Ghorofa 3 · Vitanda 102
Gharama na Ushirikiano

Gharama za Mradi na Ushirikiano wa Kimataifa

Ujenzi wa jengo utagharimu shilingi bilioni 25 za Kitanzania, na vifaa tiba na vifaa vya hospitali vitagharimu jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 25 za Kitanzania — jumla ya shilingi bilioni 50 kwa mradi wote.

Wataalamu watakaohudumia kitengo hiki wanapata mafunzo yao nchini India na Tanzania na wanapata ufadhili kutoka kwa mdau aitwae Global Heartcare Foundation.

🌍 Ushirikiano wa Kimataifa

KCMC tayari imeingia makubaliano ya ushirikiano na wadau wa kimataifa ambao wamekubali kufadhili asilimia 90 ya gharama za ujenzi. Msaada wa Watanzania wenyewe unakamilisha asilimia iliyobaki ya mradi huu wa kihistoria.

TSh 25B

Gharama za Ujenzi

TSh 25B

Gharama za Vifaa

Ushirikiano wa Kimataifa KCMC

KCMC – Ujenzi na Ushirikiano wa Kimataifa

Wito kwa Watanzania

Rai kwa Watanzania Wote — Ndani na Nje ya Nchi

Kupitia vyombo vya habari, tunatoa wito wa dhati kwa Watanzania wote popote mlipo ndani ya mipaka ya nchi yetu na nje ya nchi kuungana katika juhudi hii ya kitaifa. Huu si mradi wa KCMC pekee. Huu ni mradi wa Watanzania wote.

Ni mradi wa kulinda maisha ya ndugu zetu, wazazi wetu, watoto wetu, na vizazi vijavyo. Tunawaomba Watanzania wa kila rika na kila nafasi — vijana, wazee, wafanyabiashara, wafanyakazi, wakulima, viongozi, na diaspora yetu kuchangia kwa moyo wa uzalendo na mshikamano.

❤️

Kila mchango ni muhimu.

🌟

Kila mchango ni uhai.

🌿

Kila mchango ni tumaini.

Watanzania Wote Tuungane

"Kwa pamoja, tunaweza kujenga kituo hiki.
Kwa pamoja, tunaweza kuokoa maisha."

Changia Leo

JINSI YA KUCHANGIA

Ndugu Watanzania, Unaweza kuchangia kupitia njia zifuatazo.
Hakikisha jina la akaunti ni: KCMC MOYO

Akaunti za Benki

Bank of Africa

Namba ya Akaunti

04563580007 TSH
04563580010 USD
CRDB Bank

Namba ya Akaunti

0150686858800
NMB Bank

Namba ya Akaunti

40310194610
NBC Bank

Namba ya Akaunti

017172000770

Mitandao ya Simu

Mixx by Yas
YAS

Lipa Namba

15175376
Halotel
HaloPesa

Namba ya Wakala

23758475

Nje ya Mtandao

Mchango Ana kwa Ana

Mnakaribishwa kufika moja kwa moja katika hospitali yetu kwa msaada wa karibu.

Hospitali ya KCMC, Moshi

Tunawapokea kwa heshima kubwa

KCMC Logo

Uongozi wa Hospitali

KCMC – Kilimanjaro

Taasisi ya Shirika la Msamaria Mwema

Dar es Salaam, 09 Aprili 2026

🫀

Tuchangie Leo. Tuokoe Maisha Kesho!

Kwa pamoja, tunaweza kujenga kituo hiki.

Kwa pamoja, tunaweza kuokoa maisha.

Na kwa pamoja, tunaweza kuandika historia mpya ya huduma za afya nchini Tanzania.

Mchango wako unalindwa na uhakika wa KCMC — Taasisi ya Shirika la Msamaria Mwema, Moshi.

🫀 CHANGIA JENGO LA MOYO