2026-01-13 00:00:00
•
TIBA
•
5 min read
KURUGENZI YA TIBA INAVYOIMARISHA IDARA ZAKE
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba - KCMC Dkt. Sarah Urasa wa kwanza mkono wa kulia akiambatana na Maafisa Utumishi na Utawala ameongoza kikao na watumishi wa Idara ya Patholojia kikilenga kujadili na kupanga masuala mbalimbali ya kiutendaji kwa mwaka 2026.
Kikao hiki kimeangazia mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma za afya, kuimarisha utendaji wa idara pamoja na kuweka vipaumbele vitakavyochangia huduma bora, za kisasa na zenye ufanisi kwa wagonjwa.
Related News