KCMC NA WADAU WA AFYA WAIMARISHA USHIRIKIANO KUPITIA MRADI WA FCI
Leo, tarehe 5 Novemba 2026, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini – KCMC imepokea ugeni kutoka Ubalozi wa Marekani, Wizara ya Afya, Shirika la World Vision Tanzania pamoja na Shirika la Compassionate, kwa lengo la kujadili na kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa Mradi wa Afya wa Imani na Jamii (Faith and Community Initiative – FCI).
Katika ziara hiyo, KCMC imewasilisha shughuli na juhudi mbalimbali inazozitekeleza katika kuboresha afya ya jamii, katika maeneo ya mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu, pamoja na kuboresha huduma za lishe na afya ya mama na mtoto.
Aidha, ziara hiyo imekuwa fursa ya kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizo katika kuboresha mifumo ya utoaji huduma za afya, kuongeza uelewa wa jamii na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na endelevu za afya.
Kupitia ushirikiano huu, KCMC inaendelea kuthamini mchango wa wadau mbalimbali katika kuimarisha huduma za afya na kuboresha ustawi wa jamii.
Related Stories
2026-11-04 00:00:00
WAJUMBE WA BODI YA UTAWALA YA SHIRIKA LA MSAMARIA MWEMA (GSF)/KCMC WAFANYA ZIARA
READ ARTICLE