WAJUMBE WA BODI YA UTAWALA YA SHIRIKA LA MSAMARIA MWEMA (GSF)/KCMC WAFANYA ZIARA
Moshi, Novemba 4, 2026 – Wajumbe wa Bodi ya Utawala ya Shirika la Msamaria Mwema (GSF)/KCMC wamefanya ziara katika maeneo mbalimbali ya taasisi kwa lengo la kujionea namna huduma zinavyotolewa pamoja na maendeleo ya miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa.
Katika ziara hiyo, wajumbe walitembelea jengo la KCMC Centre of Excellence Laboratory @kcmc_coe , ambalo ujenzi wake umekamilika na kwa sasa lipo katika hatua ya usimikaji wa vifaa vitakavyotumika katika shughuli za maabara.
Akitoa historia ya mradi huo, Mkurugenzi wa Huduma za Maabara, Prof. Ireen Kiwelu (picha ya 8), aliwaeleza wajumbe safari ya mradi huo kuanzia hatua za awali hadi kukamilika kwa ujenzi wa jengo hilo, pamoja na hatua inayofuata ya maandalizi ya kuanza kutoa huduma.
Maabara hiyo inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha huduma za afya kupitia upimaji wa sampuli mbalimbali, kufanya tafiti za kisayansi na kutoa fursa za mafunzo kwa wataalamu wa afya jamii.
Related Stories
2026-11-04 00:00:00
WAJUMBE WA BODI YA UTAWALA YA SHIRIKA LA MSAMARIA MWEMA (GSF)/KCMC WAFANYA ZIARA
READ ARTICLE