Processing...

News Room

NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D

NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D
NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D
NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D
+3 More Images
NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D
NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D
Leo, tarehe 16 Septemba 2026, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini - KCMC, imeshiriki katika Mkutano wa 4 wa Mwaka wa Tiba Rekebishi (4th Annual Rehabilitation Summit), unaofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC), Dar es Salaam. Mkutano huu umefunguliwa rasmi leo na Prof. Tumaini Nagu, Naibu Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais, TAMISEMI (Afya). Kupitia ushiriki wake, KCMC imepata fursa ya kuonesha huduma na kutoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa na Idara ya Viungo Tiba na Vifaa Saidizi. Aidha, KCMC imeonesha matumizi ya teknolojia ya akili mnemba (AI) na 3D katika utengenezaji wa vifaa tiba pamoja na namna huduma hizo zinavyowasaidia watu wenye uhitaji wa huduma za urekebishaji kurejesha uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali na kuboresha maisha yao. KCMC inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuimarisha huduma za tiba rekebishi na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu huduma muhimu za afya zinazotolewa.

Related Stories

NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D
2026-09-16 00:00:00

NAMNA KCMC INAVYOTUMIA AI NA 3D

READ ARTICLE
KCMC NA TVOH YAWAANGAZIA WENYE JINSI TAT
2026-09-08 00:00:00

KCMC NA TVOH YAWAANGAZIA WENYE JINSI TAT

READ ARTICLE
KCMC, EGPAF ZAJADILI AFYA YANGU
2026-09-07 00:00:00

KCMC, EGPAF ZAJADILI AFYA YANGU

READ ARTICLE

Join the Discussion

× Preview
🫀
CHANGIA JENGO LA MOYO
Saidia Ujenzi wa Cardiovascular Centre