WAMESTAAFU LAKINI BADO WAPO NASI
Wamestaafu, lakini mchango wao unaendelea kuishi KCMC. 💙
Pichani ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha wa KCMC, CPA Hilda Mungure (katikati), pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi, Bi. Redempta Mamseri (kulia), ambao wameungana na familia ya KCMC kushuhudia uzinduzi wa Jengo la Tiba ya Mionzi.
Uwepo wao katika siku hii ya kihistoria ni ishara ya mshikamano, urithi wa uongozi bora na mchango mkubwa walioutoa katika safari ya kuijenga na kuiimarisha KCMC kwa miaka mingi.
KCMC inajivunia viongozi wake wa sasa na waliostaafu, ambao wameendelea kuwa sehemu ya historia na maendeleo ya taasisi yetu.
#KCMC #KCMCFamily #Radiotherapy #CancerCare #LeadershipLegacy AfyaBora
Related Stories