2026-01-13 00:00:00
•
ARTIFICIAL INTELLIGENCE
•
5 min read
KCMC NA AKILI MNEMBA (AI)
Hospitali ya KCMC imeandika historia mpya katika mageuzi ya huduma za afya kwa kuandaa warsha maalum ya siku 5 inayolenga Tiba ya Kidijitali na matumizi ya Akili Mnemba (AI) katika utoaji wa huduma za afya. Warsha hii muhimu inaongozwa na wataalamu kutoka Taasisi ya Tiba ya Kidijitali (Digital Institute of Health) iliyo chini ya Marburg University Hospital – Ujerumani.
Warsha hii imewakutanisha madaktari kutoka idara mbalimbali za hospitali, wakiwemo madaktari bingwa na madaktari wanaoendelea na mafunzo (residents) kutoka Idara ya Huduma za Dharura, Uzazi na Magonjwa ya Wanawake, Magonjwa ya Ngozi na Zinaa, Watoto pamoja na wataalamu wa Epidemiolojia na Biostatistiki.
Lengo kuu la warsha hii ni kujenga uwezo wa utekelezaji wa vitendo wa akili mnemba (AI) na tiba kwa njia ya mtandao (Telemedicine) katika huduma za kila siku za kliniki, sambamba na kufungua fursa za utafiti kwa wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters). Kupitia mafunzo haya, washiriki wanajengewa uelewa wa namna teknolojia inavyoweza kusaidia kufanya maamuzi ya kitabibu kwa haraka, kuongeza usahihi wa huduma na hatimaye kuboresha ubora wa huduma kwa wagonjwa.
Related News