Processing...

2025-12-19 00:00:00 IBADA 5 min read

TUMEUONA MKONO WA MUNGU WENYE NGUVU

Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini – Baba Askofu Dkt. Fredrick O. Shoo leo tarehe 19/12/2025, ameongoza Ibada ya Shukrani ya Sikukuu ya Krismasi KCMC, ibada ya kipekee iliyojaa baraka, shukrani na mshikamano mkubwa wa familia ya GSF/KCMC. Watumishi wa GSF/KCMC huadhimisha siku hii kila mwaka wiki moja kabla ya tarehe 25 Desemba, kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa uhai, huduma na mafanikio katika mwaka mzima wa kuwahudumia wagonjwa na jamii kwa ujumla. Ibada ya mwaka huu imekuwa ya kipekee zaidi, ikihusisha matukio mbalimbali, baadhi yakiwa ya mara ya kwanza kufanyika, yakiwemo: ✅ Zawadi kwa wapambaji bora wa idara mbalimbali za hospitali waliopamba kwa ubunifu na jumbe zenye kuakisi maana ya Krismasi. ✅Zawadi na pongezi kwa watumishi wanaostaafu, kama ishara ya shukrani kwa huduma yao ya uaminifu. ✅Kutambua na kutoa zawadi kwa vinara wa uchangiaji damu, waliogusa na kuokoa maisha ya wengi. ✅Pongezi kwa watumishi waliomaliza masomo, kuenzi juhudi zao za kujiendeleza kitaaluma. ✅Furaha na tabasamu kutoka kwa Father Christmas, aliyegawa zawadi na kuleta shamrashamra. ✅Na kubwa zaidi, chai na chakula kilichoandaliwa na hospitali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, na kugawanywa kwa wagonjwa, ndugu wa wagonjwa pamoja na watumishi, kama ishara ya upendo na mshikamano wa kweli wa Krismasi. Siku hii imejawa na shukrani, furaha, upendo na matumaini mapya, ikitukumbusha dhamira yetu ya kuendelea kuhudumia kwa moyo wa huruma na utu.

Related News

Medical technology
2025-12-20 00:00:00

WALIOMALIZA MASOMO WAMSHUKURU MUNGU

Read Story →
Medical technology
2025-12-20 00:00:00

WAMALIZA UTUMISHI ULIOTUKUKA

Read Story →
Medical technology
2025-12-19 00:00:00

TUMEUONA MKONO WA MUNGU WENYE NGUVU

Read Story →

Leave a Comment