2025-11-07 00:00:00
•
HUDUMA
•
5 min read
SHIDA YA AFYA YA AKILI IPO TANZANIA
Hospitali ya KCMC inaendelea kufanya mageuzi ya huduma za afya nchini, hususan katika eneo la afya ya akili lililodumu kwa muda mrefu kwa kutokupewa kipaumbele. Kupitia kongamano la 16 la “Focus on Mental Health” linalofanyika Novemba 7-8, 2025 katika ukumbi wa Uhuru Hostel, Moshi, KCMC imeungana na wadau mbalimbali wa afya, wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi, vyuo vikuu, taasisi za utafiti, wanafunzi na wanaharakati wa afya kuendelea kujadili mustakabali wa huduma za afya ya akili nchini Tanzania, chini ya kauli mbiu 'Learning From Our Neighbours'.
Mgeni Rasmi wa kongamano hili ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Dkt. Jairy Khanga, amepongeza jitihada za KCMC na kufungua rasmi kongamano hili kwa kusisitiza kuwa wakati huu ambapo changamoto za afya ya akili zimeongezeka kwa kasi KCMC imeonesha njia sahihi inayotakiwa kuigwa na taasisi katika mikoa mingine. Ameeleza kuwa sekta ya afya ya akili sio ya wataalamu pekee bali ni jukumu la jamii yote, taasisi zote na ofisi zote zinazogusa maisha ya binadamu.
Katika hotuba yake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC Dkt. Sarah Urasa ameelezea safari ya KCMC katika kuijenga idara hii kutoka sifuri hadi kuwa idara kamili. Mwaka 2018 KCMC haikua na psychiatrist hata mmoja leo ina wataalamu 6 pamoja na wanasomea super specialization, ina clinical psychologist, occupational therapists na inakamilisha mpango wa kuanzisha mafunzo ya postgraduate psychiatry yatakayofanyika hapa hapa KCMC. Pia kupitia ushirikiano na Duke University (Marekani), Radboud University (Netherlands) na Newcastle University (England) KCMC imeanzisha telehealth counselling hub inayowezesha wataalamu kutoa huduma za ushauri nasaha kwa wagonjwa waliopo kwenye vituo vya afya katika jamii na maeneo ya mbali, ikishughulika na changamoto kama depression na suicidal ideation.
Aidha, mmoja wa washiriki wa kongamano hili amepongeza hatua za KCMC kwa kuandaa kongamano hili muhimu akieleza kuwa limempa mtazamo mpana, litawasaidia kuongeza maarifa na kwenda kuwasaidia wananchi kwenye maeneo wanayotoka. Ameeleza kuwa kongamano kama hili linabadilisha fikra, linavunja unyanyapaa, na linakuza ujasiri wa watu kutafuta huduma za kitaalamu badala ya kukaa kimya.
Related News