Loading...

2025-10-17 00:00:00 β€’ SERVICE β€’ 5 min read

KCMC YAZINDUA PRIVATE CLINIC

Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Research data
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC leo imezindua eneo maalum la Kliniki Binafsi (Private Clinic), litakalotumika kwa wagonjwa wanaotumia bima mbalimbali pamoja na wale wanaolipa kwa fedha taslimu (cash). Hafla ya uzinduzi wa kliniki hiyo imefanyika kwa ibada ya kutiq wakfu iliyohudhuriwa na viongozi wa Bodi ya GSF/KCMC, wachungaji, wakurugenzi, viongozi wa idara mbalimbali pamoja na watumishi wa hospitali. Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa Nje (OPD), Dkt. Tumaini Mirai, alieleza faida za kliniki hiyo binafsi, akibainisha kuwa wagonjwa watapata huduma zote muhimu kwa muda mfupi bila kuhangaika kutoka sehemu moja hadi nyingine. β€œNdani ya eneo hili, mgonjwa ataweza kuonana na daktari, kupata huduma za maabara, vipimo vya moyo na huduma za famasi,” alisema Dkt. Miray. Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Prof. Gileard Masenga, alitoa pongezi kwa wataalamu wote waliobuni na kuandaa wazo hili, akisema kuwa jambo lililoonekana gumu awali sasa limekuwa halisi kutokana na maono, ushirikiano na juhudi za pamoja. β€œLeo tupo hapa kushuhudia matunda ya ubunifu na kujituma kwa timu yetu.” alisema Prof. Masenga. Aidha, Meneja wa Bima wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Fikirini Mkwabi alipongeza hatua hiyo ya KCMC, akisema kliniki binafsi itarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanufaika wa bima, hususan wateja wa NHIF ambao awali walikuwa wanakosa huduma fulani kutokana na ufinyu wa nafasi au muda. Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Mchungaji Canon Dkt. Moses Matonya- Katibu Mkuu wa CCT na Mjumbe wa Bodi ya GSF ambaye ameongoza zoezi la kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa eneo hilo jipya. Dkt. Matonya aliipongeza KCMC kwa hatua hiyo muhimu na kueleza kuwa, uamuzi wa kuanzisha kliniki binafsi ni ishara ya ubunifu, ufanisi, na kujituma katika kuboresha huduma kwa wananchi. Aliongeza kuwa, hatua hiyo ni matokeo ya maono makubwa ya uongozi wa KCMC katika kuhakikisha kila mgonjwa anapata huduma bora kwa wakati. Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya KCMC, Dkt. Adeline Kimambo, alipata nafasi ya kutoa neno la shukrani ambapo alianza kwa kumshukuru Mungu kwa kufanikisha hatua hiyo muhimu, akisisitiza kuwa mafanikio hayo hayakuja kwa juhudi za kibinadamu pekee bali kwa neema na msaada wa Mungu.

Related News

Medical technology
2025-10-17 00:00:00

KCMC YAZINDUA PRIVATE CLINIC

Read Story β†’
Medical technology
2025-09-10 00:00:00

KCMC ITAPENDEZA NA CORAL PAINT

Read Story β†’
Medical technology
2025-09-10 00:00:00

KCMC NA DUKE WAMLETA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA

Read Story β†’

Leave a Comment