2025-09-10 00:00:00
•
MANAGEMENT
•
5 min read
KCMC NA DUKE WAMLETA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA
Uongozi wa hospitali ya KCMC ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaria Mwema – GSF na Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Prof. Gileard Masenga leo tarehe 10/09/2025 umepokea ugeni wa Kaimu Balozi wa marekani nchini Tanzania Mhe. Andy Lentz.
Katika ziara yake, Balozi Lentz ametembelea na kujionea ushirikiano wa KCMC na Duke unavyofanyakazi chini ya Prof. Blandina Mmbaga na Dkt. Dorothy Dow. Ziara hii imelenga kujifunza zaidi kuhusu tafiti bunifu zinazotekelezwa katika ushirikiano huu zinavyoleta mchango mkubwa katika maendeleo ya huduma za afya na tafiti barani Afrika.
Mheshimiwa Balozi alipata nafasi ya kujifunza kuhusu mafanikio ya tafiti zinazofanywa na wataalamu wetu akiwemo:
🔹 Dkt. James Ngocho (mshindi wa tuzo ya K43)
🔹 Dkt. Francis Sakita (Mkuu wa Idara ya Dharura - KCMC)
🔹 Dkt. Kim Madundo (Mkuu wa Idara ya Afya ya Akili - KCMC)
🔹 Prof. Blandina Mmbaga (Mkurugenzi wa KCRI na kiongozi mwenza wa KCMC-Duke Collaboration)
🔹 Dkt. Dorothy Dow (kiongozi mwenza wa KCMC-Duke Collaboration).
Related News


