2025-09-10 00:00:00
•
MANAGEMENT
•
5 min read
KCMC ITAPENDEZA NA CORAL PAINT
Hospitali ya KCMC imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma na miundombinu yake. Leo tarehe 10/09/2025 KCMC imepokea wageni kutoka INSIGNIA Ltd (Coral Paint) wakiongozwa na Meneja wao kwa Mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Lusajo Mwambene, na kutoa msaada wa rangi kwa ajili ya kuboresha mandhari na miundombinu ya hospitali.
Katika tukio hili, Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC Prof. Gileard Masenga amewashukuru kwa moyo wa upendo na mshikamano waliouonyesha kupitia msaada huu ambao unaambatana na mafunzo ya kuongeza ujuzi wa mbinu za kisasa za upakaji rangi kwa wataalamu wetu wa rangi hapa KCMC.
Related News


